Historia ya Sheikh Salim Mti Mkavu
Namshukuru
Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kunijaalia fikra na utashi wa kuandika kitabu hiki nilichokitambulisha
kwa jina la سيرة
ملهمة (siiratun
mulhimah)
.Makusudio
yangu makubwa katika kuandika kitabu hiki ni kuelezea sifa na mwenendo wa maisha ya Bwana na walii aliye kipenzi cha Mwenyezi
Mungu Mtukufu na Mtume (SAW).
Ni Matarajio
yetu Historia hii tuliyoiandika ndani ya kitabu hiki itahifadhika na kujenga kumbukumbu
juu ya maisha ya watu wema
kwa ujumla. Kuwakumbuka watu wema na kufuatisha matendo mema ni ufunguo wa kheri hapa
duniani na Akhera.
Insha Allah
Mwenyezi Mungu amjaalie kila la kheri msomaji wa kitabu hiki na amjaalie kuwa na matendo
mema.
“Eee Mwenyezi
Mungu tujaalie sote
mwishilio
mwema na utujaalie kuwa
watu
wa peponi”
(Aamiin).
Sura
ya kwanza:
Asili Yake
|
Ninayekusudia kumhadithia historia yake
ndani ya kijitabu hiki jina lake halisi ni Sheikh Salim Ibn Mubaarak Ibn
Salim Al- Gahlan. Asili yake ni mwarabu wa asili ya Hazramuut nchini
Yemen anayetokana na uzazi wa Sheikh Mubaarak Ibn Salim Al-Gahlan
na mama yake Bibi Fatimah. Sheikh Salim amezaliwa nchini Kenya katika
mji wa Mombasa kitongoji cha Bondeni mnamo mwezi February mwaka 1922. Kama ilivyokuwa mash huri na
kawaida kwa waja wema wa Mwenyezi Mungu maisha yao hukumbwa na hali na matukio
tofauti tofauti ambayo huwa ni bishara na alama za utukufu wao katika maisha
yao ya kidini.

Sheikh
Salim Mubarak Salim Gahlan
Vivyo hivyo Sheikh Salim amepitia
katika joto hilo, ikiwa ni ishara kwa wenye akili kutambua utukufu wa darja ya
bwana huyu mbele ya viumbe vya Allah.
Sura
ya pili
Malezi
yake
|
Bishara hii ilianza kuonekana pale wazazi wake wote wawili kufariki
angali mdogo sana na kupelekea kulelewa na babu yake Sheikh Salim Gah Lan na
bibi yake upande wa mama yake Bi Sahale binti Khamisi aliyekuwa akiishi kijiji
cha Sarigoi Mjini Mombasa.
Hata hivyo babu yake hakumlea muda
mrefu akafariki akimuacha Sheikh Saalim chini ya mikono ya bibi yake kwa mama
yake Bi Sahale akiwa bado mdogo sana. Hata hivyo bibi yake huyo ( yaani Bi
Sahale Binti Khamisi) naye hakikupita kipindi kirefu naye akafariki( hiyo
ilikuwa mwaka 1948) akimmwacha sheikh angali mdogo kiumri.
Kutokana na kifo cha bibi yake,
nafasi ya malezi yake ilishikwa na mjomba wake bwana Mansuri Bin Abdallah.
Vivyo hivyo mjomba wake haikupita muda
mrefu naye akafariki baada ya kumlea masiku machache.
Baada ya kifo cha mjomba wake
Mansuri, suala la malezi yake lilikuwa ni swali lililogonga vichwa vya
wanandugu hata asijue hata mmoja vipi itakuwa malezi yake baada ya kifo cha
mjomba wake. Hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipodhihirisha yale yaliyofichikana
katika masaibu na mikasa mbalimbali iliyomkumba Sheikh Salim katika makuzi
yake.
Lakini kwa rehma na muongozo wa Allah,
Sheikh Sharifu Al Habib Swaleh Izzadin ( radhwia llah anhu) alimchukua Sheikh
Salim kwa ajili ya kumlea. Wal hamdulillah hapo ndipo ilipopatikana nafasi
kubwa kwa Sheikh Salim kujifunza mambo mbalimbali yausuyo dini ya uislam na
twariqa kwa ujumla
Sura
ya Tatu
Elimu
na masheikh zake
|
Sheikh Salim Mubarak alipata bahati ya kuwa
katika kizazi cha wajuzi wa dini. Hii ni kumaanisha kuwa baba yake mzazi Sheikh
Mubarak Bin Salim alikuwa ni miongoni mwa wanazuoni jambo lilimsaidia Sheikh
Salim kujiegemeza katika kujifunza dini yake tokea utotoni mwake.
Na hii huwa ni kawaida kwa wenye
akili kuwa malezi na mafundisho mema kwa mtoto huanza kwa wazazi wake. Baada ya
kuishi muda mdogo na wazazi wake sheikh salim alichukuliwa na babu yake
aliyekuwa rafiki wa karibu wa Sheikh Swaleh Izzadin.
Vile vile naye babu yake Sheikh
Salim Gahlan naye alikuwa ni miongoni mwa wanazuoni wa kiislam waliokuwa
wakiheshimiwa katika zama zake. Hivyo pia Sheikh Saalim alipata nafasi ya
kujifunza mas ala kwa babu yake. Baada ya kuondokewa na babu yake na baadae
mjomba wake, Sheikh Salim alichukuliwa na Sharifu, Alhabib Sheikh Swaleh
Izzadin ambaye ndiye mwalimu wake mkubwa aliyepata kutoka kwake elimu ya dini yake.
Hapo ndipo ndipo malezi ya Sheikh
Salim yakawa yamelenga zaidi tassawf kwa mafunzo ya kiroho, kimwili, na
uchamungu kutoka kwa Al Habib Sharif Swaleh Izzadin Al Jailaniy. Hata hivyo
elimu yake ilitoka kwa wanazuoni wengi zaidi ya hapa kwani baadae alipitia
katika mikono salama yenye kuijua dini mpaka kufikia hadhi ya kuwa khalifa na sheikh.
Miongoni mwa masheikh zake Alhabib
Salim Mti Mkavu ni:-
1.Al Habib Sheikh Sharif Swaleh
Izzadin
2. Sheikh Salim Gah lan
3. Sheikh Mubarak Bin Salim ( Baba
Yake)
4. Al Habib Sheikh Sharif Muh Dhari
5. Al Habib Sheikh Omari Bin Alli
Kullatein
6. Sheikh Sufi Bin Kabole
Sura
ya Nne
Kuanzishwa
kwa Madrasa ya Izzadin
|
Kama alivyochukuliwa sayyid Sheikh Abdul Qaadir Jai Laany na Nabii
Khidri kumpeleka Baghdad kwa ajili ya kupata elimu vivyo hivyo ndivyo alivyo
fanya Sheikh Sharif Swaleh Izzadin kwa Sheikh Saalim. Baada ya kulitekeleza
jambo hilo Sheikh Izzadin alimtoa Sheikh Salim katika mji wa Mombasa kumpeleka
hadi Moshi nchini Tanzania kabla ya uhuru.
Baada ya kumtoa sheikh salim katika
mji aliozaliwa mombasa alimpeleka katika
mji wa moshi na akapafanya hapo ndio makazi ya sheikh salim. Baadaye sharifu
swalehe akahama katika mji wa moshi akamuusia sheikh saalim kubaki hjapo katika
zawiya ya moshi mjini.
Kilipita kipindi kirefu tangu
sharifu swlalehe ahame moshi na kumuacha sheykh salim zawiyani.kwa vile sheykh
salim alikua na mapenzi makubwa sheykh wake sharifu swaleh basi ikambidi
amuombe idhini ili amfuate akaishi naye tena kwani alifurahi kuwa naye karibu
zaidi na zaidi.
Alipomfikishia ombi la kutaka
kumfuaata,sharifu swalehe akamwambia'kaa
Hapo Hapo Moshi Na Ufungue Madrassa Ya Kusomesha Watoto Na Darsa
Utakalolifungua Uliite Madrasat-Izzadin' alipopata
jibu hili sheykh salim hakusononeka bali alitia bidii juu ya amri aliyopewa na
mara moja akafungua darsa katika zawiya ya pasua hapo hapo mjini moshi.
Akaendelea kudar-sisha hapo zawiyani
pasua kwa muda kiasi,ndipo alipoombwa na shaushi khamisi lelo wa njoro hapo
hapo moshi ahame kutoka alipokua akiishi zawiyani pasua na ahamie njoro.
Chuo
cha Izzadini tawi no 2
Shaushi khamisi lelo alimuahidi
sheykh salim kua atamuandalia pahala pake pa kukaa katika katika nyumba
yake,pia atatoa nafasi kwa ajili ya madrassa.
Sheikh salim alipoombwa hivi
hakukataa bali alihama katka zawiya ya pasua na akahamia njoro kwa
shaushi khamisi lelo na akafungua dar-sa akawa anasomesha dini.
Mpaka anapokea amri kuanza kusomesha
wanafunzi,sheikh salim alikua amepata elimu kwa namna kadhaa,kama vile
mafundisho ya ana kwa ana na sharifu swaleh au akasomeshwa kwa ishara.pia
alipambanukiwa na jambo lolote liwe la kidunia au dini kwa namna alivyoitaka mwenyezi mungu
mwenyewe. Na bila shaka huo ndio utaratibu waupatao mawalii wa mwenyezimungu.je
haijakupambanukia tu kujua kuwa bwana huyu dar-ja yake iko vipi?
Akiwa amefungua dar-sa na
anafundisha wanafunzi wake hapo njoro dar-sa yake ilipanuka ikatokea kuwa
miongoni mwa dar-sa.na kwa kipindi chote
hicho hakuwahi kutembelewa na mlezi wake waroho sharifu swalehe.
Basi ilipotimia wakati,sharifu
swalehe akaja moshi. Kuja kwwake moshi haikuwa bure ila alikuja kwa amri ya
mwenyezi mungu. Kwa vile yeye sheikh swaleh ndiye aliyemgundua sheikh salim
kuwa ni mwenye darja katika dini, basi mwenyezi mungu akamuamrisha sharifu
swaleh aende moshi akambashirie sheikh salim ajijue yeye ni mtu wa cheo gani
mbele ya waumini. Sheikh salim akiwa darasani kwake njoro akiendelea kusomesha
alipata khabari kuwa sharif swaleh amekuja.
Sura ya Tano
Kifo cha Sharifu Swaleh Izzadin
(r.a)
|
Hapoapo bila simile akatoka hima darasani
kwake na akamuwahi sharifu swaleh zawiyani alipoifikia. Sheikh salim
alipomtokezea sharif swaleh machoni pake, hapo sharif swaleh akatabasamu na
akaita, kumuita sheikh salim akasema" yaa salim bahati yako kubwa" na
hapo sharifu swaleh akiwa na hali ya kuumwa akatia fatha nma akaomba dua kwa
muda mrefu sana il hali kamuelekea sheikh salim kisha akamruhusu atoke nje.
Siku ya pili yake sharif swaleh akafdariki dunia, huo ukiwa ni mwaka 1968.
Ulikuwa ni msiba mzito sio kwa sheikh salim tu bali kwa muridi na waislam wote
wananomfahamu na wasiomfahamu sharif swaleh.
Ulizima moyo wa sheikh salim mzizimo
wote wa huzuni huku akifarijiwa na sharif muhdhar bin hussein al ahdaly ambaye
pia ni mpenzi na ndugu kisha khalifa wa sharifu swaleh akamnasihi akamwambia
huzunika kwa msiba wa kuondokewa na sharif swaleh, lakini liwazika na radhi
alizokupa sharif swaleh na wala hata twezeka hapo dunianio. Maliwazo hayo
yalitoka moyoni mwa sharifu muhdhari kumliwaza sheikh salim. Haikutoshea kwa
sharifu muhdhari kumliwaza sheikh salim kwa maneno hayo tu balio naye akamfanya
kama mwanae na akawanadia wanae wasimtenge sheikh salim kwa jambo lolote
litakalofanywa katika familia ya sharifu muhdhari bin husein al ahdany
Anahadithia mwenyewe sheikh salim
kuwa tangu alipo husia sharifu muhdhari kwa wanawe hapajakengeukwa kwa hata
kidogo mpaka sasa. Baada kuisha kupita huzuni hiyo sheikh salim akaendelea
kudarsisha kwa bidii zaisdi ahata wakati mmoja akawafikia mgeni kutoka
zanbzibar. Huyo alikuwa sharifu omar bin alliy kulltayn. Lengo la safari ya
sheikh omari bin ally toka zanzibar na kuja moshi ni kumzuru sharifu swaaleh
izzadin. Basi sharifu omary bin ally kullatayn akifuatana na sheikh salim na
jamaa wengine wakaenda hadi kwenye kaburi la sharif swaleh kumzuru.
Baada kuisha kumzuru sharif swaaleh wakarudi
na wakaenda moja kwa moja nyumbani kwa sharif muhdhar. Walipofika nyumbani kwa
sharifu muhdhari wakatmkuta sharifu muhdhari yupo mlangoni pake anawasubiri.
Walipofika nyumbani aliposimama sharifu muhdhari akaita kwa sauti kubwa."
yaa salim nilikuwa na sharif swaleh hapa na maeniagiza ni kwambie kuwa wewe ni
khalifa na tena ni sheikh na tena uko juu juu juu" kisha sharifu muhdhari
akatia fat ha na akaomba dua hal;afu akawaeleza waliohudhuria kuwa tangu sasa
salimu ni khalifa na ni sheikh hivi ndivyo sheikh salim alivyopata ukahalifa na
usheikh pia.
Cheo alichonacho hakupewa kwa utashi wa mtu
bali mwenyezi mungu aliridhia malezi aliyopata kwa mabwana wakubwa hawa na
akawaridhia muda ukufika wamkabidhi cheo chake. Baada ya hayo kutendeka,
haukupita muda mrefu haukupita muda mrefu sheikh muhdhar naye akafariki. Hii
inaonyesha jinsi ambavyo kila aliyemlea sheikh salim alikuwa na kazi
alizopangia na mwenyezi mungu kuzifanya na kakisha timiza aliloagizwa basi huwa
hana buni ila kumuachia mwingine.
Tizama wazazi wake walipo mzaa
sheikh saalim jukumu lao likawa liometimia. Ulezi wa awali ukawansibikia babu
na bibi yake. Nao kiasi cha ulezi wao kwa sheikh salim kilipotimia fursa ya
malezi ikatawaliwa na mjomba wake. Naye jambo lake lilipotimia kwa malezi ya
kawaida ndipo malezi ya kiroho yakawa mikononi mwa watukufu wa darja. Hivi
ndivyo alivyopanga mwenyezi mungu na wala si utashi wakiumbe yeyote bali
majaliwa yake allah. Sheikh salim amelelewa ndani ya bahari ya twarika. Sheikh
salim kazaliwa ndani ya twarika na anaishi ndani ya twarika. Kwa ajili hiyo
basi hapana shaka yeyete juu ya malezi yake.
Sheikh salima liondoka katika mji
aliyozaliwa kwa amri ya kheir toka kwa allah juu ya sharif swaleh akakaa zawiyani
na akuondoka mahala hapo ila kwa amri ya kheri toka kwa allah juu ya sheikh
swaleh kumtaka sheikh salim fafungue darsa darsa l;a kusomesha elim ya dini kwa
muongozo wa kitwarika. Ndipo sheikh salim alip[o fungua darsa na kusomesha. Kwa
vile kalelewa katika mazingira ya kheiri na kweli na yeye kachaguliwa na
mwenyezi mungu katika kuyahifadhi mafundisho mema , basi hakufanya jambo ila
katika kuyahifadhi mafundisho mema basi hakufanya jambo ila mpaka apte ruksa
maalum toka kwa mabwana wakubwa. Sasa namna avyopata habari allah anajua.
Sura ya Sita
Kuhamia Arusha Sheikh Saalim
|
Haukupita muda baada ya kifo cha
sharifu muhdhari akaja mcha mungu mmoja mwenye asili ya kisomali akiitwa Sheikh
Sufi Kabole ameendewa na sharifu swaleh amemuagiza Sheikh Sufi Kabole amchukue
kutoka moshi ampeleke arusha na awe na yeye na amjengee sheikh salim zawiya
yake mtaa wa Ngarenaro Arusha.
Sheikh Salim alipoambiwa amri hii
toka kwa sheikh wake sharifu swaleh hakuwa na budi ila aliomba dua kwa mwenyezi
mungu ili aimarishe madrasa aliyokuwa ameifungua moshi; madrasat izzadini
awaswadifishe vifuani mwao muri wote wa sharifu swalehe hapo moshi na wadumu
ndani ya twarika zaidi na zaidi kisha akwaaga waislam muridi wa moshi pamoja na
wanafunzi wake akaondoka kwenda arusha akiambatana na sheikh sufi kabole kama
alivyoagizwa na sharifu swaleh kupitia kwa huyo Sheikh Kabole. Sheikh Salim alipofika
arusha akawa amemuegama akawa amemuegama sheikh sufi kabole, naye sheikh sufi
kabole akatimiza yote aliyoagizwa na Sharif Swaaleh juu ya Sheikh Salim.
Kisha akamuomba ruksa arejee zake mombasa
kwani yote aliyoamriwa na allah juu ya Sharifu Swaleh kumtekelezea sheikh salim
ametimiza hivyo anarudi mombasa. Sheikh salim kama ilivyokuwa wachamungu japo
wapende vipi hawazuilii haki ya yeyote mbele ya allah, hivyo akamruhusu sheikh
sufi kabole aende zake mombasa naye abaki arusha akiendeleza twarika.
Sheikh sufi kabole alipofika mombasa
naye hakukaa muda akafariki dunia. Kufariki kwa sheikh sufi kabole kuliamsha
ari na bidii kubwa ndani ya nafsi ya sheikh salim akaongeza jitihada kutimiza
kile alichotarajiwa kukifanya ndani ya uislam na twarika kwa ujumla
Bila kukawia akaanza kufundisha
madrasa msikiti wa mondeni na majlisul ulaa kwa mama betii, vilevile akawa
akifanya kila jitihada katika kuleza twarika hadi pakajengeka ilipo zawia kuu
hivi sasa matejoo-ngarenaro-arusha mjini.
Sheikh salim kafanya hayo akitarajia
rehma za mwenyezi mungu na baraka za Assayyid Sheikh Abdul Qaadir na radhi za
mabwana wa kubwa waliomlea na kumtukuza kimwili na kiroho . Katika kipindi
hicho chote mpaka mimi kuchukua jukumu la kuyaandika haya sheikh salim hakuacha
kuwa ni mwenye kuizuru madrasa aliyoicha mjini moshi chini ya mwanafuzi wake Sheikh
Ramadhani Bin Khamis Ally.
Hadi
leo madrasa ya izzadini imeweza kueneza matawi sehemu yote ya Tanzania bara na
visiwani ikiwa na idadi ya matawi zaidi ya thelathini na tano yaliyo hai.
Madrasa ya izaadini imetoa wanazuoni wengi kupitia athari ya elimu aliyoicha
sheikh salim kwa baraka za masheikh na walezi wake wa kiroho.
Sura ya Saba
Kueneza Dini na Twariqa
|
Katika
maisha ya sheikh Saalim alitumia muda wake mwingi kueneza na kuwafunza watu
dini na twariqa. Hii ilikuwa sunna ya mtukufu wa darja mtume Muhammad ﷺ na ndio mafunzo na amri aliyopewa na sheikh wake Sharif
Swaaleh(Q.A.S).
Hivyo
Sheikh Saalim alijikita katika kueneza dini na twariqa kwa harakati mbalimbali.
Miongoni mwa harakati hizo ni pamoja na ujenzi na ufunguzi wa miskiti, madrasa,
vyuo vya dini na zawia mbalimbali. Sheikh salim kupitia Twariiqatul Qaadiriyyah
Arraaziqiyyah ameweza kufungua mazawia na majaalis za kidini katika mikoa
takriban yote ya Tanzania.
Madrasa
na misikkiti ndio idadi yake haisemekani kwani mbali na madrasa nyingine
madrasa yake ya kwanza (Izzadin) ina takriban matawi yasiyo pungua thelathini
na tano nchi nzima.
Kwa
juhudi zake binafsi na kwa msaada wa
makhalifa wake ambao ndio washauri wake wakuu, sheikh salim aliweza
kuisajili taasisi ya Twariiqatul Qaadiriyyah Arraaziqiyyah Al-jailaaniyyah kwa
serikali ya Tanzania kama taasisi ya dini nchini.
Sheikh
Saalim katika harakati zake ameweza kusilimisha mamia kwa maelfu ya watu hasa
katika mikoa ya Singida, Tabora, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Dar es
salaam.Sheikh Salim hakuwa msilimishaji tu bali alihakikisha alio wasilimisha
wanapata elimu ya muongozo wa kiislam.
Mbali
na yote hayo Sheikh Salim aliyejaa hikma, elimu, maarifa na karama ni muandishi
na mtunzi mzuri na hodari wa vitabu vya
dini ya uislamu. Yote hii ni kwa ajili ya kuwagawia watu elimu mbali na njia
yake ya asili aliyorithi kwa masheikh zake ya kudarsisha. Moja ya vitabu maarufu
alivyotunga ni ALGHAUTHUL AADHWAM alichosimulia ndani yake maisha ya Sheikh
Abdul qaadir Jailaaniy (Q.A.S)
Kwa
uchache hii ndio khabari ihusuyo maisha ya bwana mkubwa wetu Swahibu Sujjadah.
والله أعلم والموافق في طريق المستقيم
Ust
Musa Abdul Rahman Msele
Comments
Post a Comment